Mitandao ya kijamii ni suala kumwa na lenye umaarufu sana kwasasa, mitandao ya kijamii ni baathi ya njia rahisi ambayo inampa mtu uwezo wa kujifunza mambo mengi na mapya, kukutana na marafiki pia inasaidia kurahisisha mawasiliano baina ya mtu na mtu/kikundi cha watu. Pia zipo baadhi ya hasara ziletwazo na mitandao ya kijamii kubwa zaidi ni mitandao isipotumiwa ipasavyo inachangia mmomonyoko wa maadili, hupoteza muda wa mtumiaji asiyejidhibiti.
Ipo mitandao mingi ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Emails, WhatsApp, Instagram, Blogs, Badoo, BBM, n.k
Mafunzo ya mitandao ya kijamii ni mafunzo yatolewayo bure kabisa na shirika lisilo la kiserikali (NGO) liitwalo Mbeya Living Lab ambapo watu wanapata nafasi ya kujifunza mitandao kama vile Google mail, Facebook, Twitter, na Blogs.
Dhumuni la mafunzo hayo nikuleta mabadiliko katika jamii yetu inayotuzunguka na kuleta mwanga katika kutumia intaneti kwa matumizi chanya ili kuleta ufanisi katika tasnia mbalimbali.
 |
No comments:
Post a Comment