Saturday, 4 October 2014

UJASIRIAMALI NI NINI??



Ujasiriamali kama somo limetokea kupendwa nawengi hasa katika jamii ya kisasa ya sasa, lakini ni watu wachache wanaojua nini hasa maana ya ujasiriamali,

-Mjasiriamali ni nani?  

-Chimbuko la ujasiriamali ni wapi?, 

-Zipi ni sifa za mjasiriamali?, 

-Nini mchango kwa mjasiriamali katika maendeleo ya Taifa?, 

-Je faida za kuwa mjasiriamali ni zipi?. 

Ukijiuliza maswali hayo utagundua kuwa kuna umuhimu wa kujifunza zaidi juu ya ujasiriamali. Ujasiriamali ni nyanja ambayo ikitiliwa mkazo inaweza leta mapinduzi katika ukuwaji wa uchumi,teknolojia,siasa na utamaduni wa jamii husika.

UJASIRIAMALI TANZANIA
Katika muktadha wa Tanzania ujasiriamali kama zana ya msingi katikaka kukuza uchumi bado haujapewa kipaumbele kwani wadau na washika dau bado hawajaweka mtazamo chanya na nguvu katika kuto elimu ya ujasiriamali kwa wananchi. Watanzania wengi wamekosa elimu hasa elimu ya mfumo rasmi(darasani) lakini elimu ya ujasiriamali inaweza tolewa popote bila hata kufuata mfumo rasmi na ikawafikia watu wengi nao wakanufaika.

Nyanja hii ya ujasiriamali imefanyiwa utafuiti na kuandikwa na kujadiliwa na wanazuoni na wasomi mbalimbali lengo ni kufanya ujasiriamali kuwa muhimili unaojitegemea ambao unaweza kutengeneza fulsa za kimaendeleo.

Wazo la ujasiriamali lilianzishwa mnamo miaka ya 1700,  Maana iliyotolewa kipindi hicho kuhusu Ujasiliamali inanguvu japokuwa kuna maana nyingi zimekwisha tolewa na zinaendelea kutolewa. Hapo mwanzo UJASIRIAMALI ulijulikana kama ni "kitendo cha kuanzisha biashara"lakini wanauchumi wengi wanaamini ujasiriamali una maana zaidi ya hapo.

Baadhi ya wanauchumi wanaona kuwa mjasiriamali ni mtu ambaye yupo tayari kuthubutu au kuanzisha jambo jipya ambalo litampa faida au litakuwa na nafasi ya kumpa faida hapo daadaye. Lakini wengine wanadai kuwa mjasiriamali ni mbunifu ambaye ubunifu wake anaunadi na kuutumia ili apate faida. Wengine wanasema "mjasiriamali anabuni bidhaa mpya au njia mpya ya uzalishaji wa bidhaa ambayo soka linahitaji bidhaa hiyo au hiduma hiyo ambayo haijapata kusambazwa hapo kabla".

Mnamo karne ya 20 mwanauchumi Joseph compete (1883-1950) anamtazama mjasiriamali kama"mvumbuzi , mbunifu ,anayeleta mageuzi na mabadiriko".Compete anaendelea kusema "mjasiriamali anamsukumo wa ubunifu , mjasiriamali anabeba mchanganyiko mpya ambao unatoa nafasi au kusaidia viwanda vya zamani kubadirika na kuwa na mfumo mpya wa kuzalisha , kufanya biashara na kutoa huduma.

Mtaalamu wa biashara Peter Drunker anaendeleza wazo hili kwa kusema kuwa "mjasiriamali ni mtu ambaye kiukweli anatafiti kwa lengo la kuleta mabadiriko na anawajibika katika mabadiriko hayo,pia anatumia mabadirko kama changamoto katika kujiletea tija na ufanisi katika kazi zake" kwa ujumla tunaweza kusema kuwa UJASILIAMALI ni kitendo cha kuchukua hatua na kuanzisha kitu (biashara) kipya au kufanya jambo ambalo linafanywa na wengine lakini katika njia tofauti huku ubunifu na mipango thabiti inayoambatana na ujasiri pamoja na msukumo wa dhati wa kufanya kazkwa didii ukiwa ndani ya mjasiriamili mwenyewe.

Wanauchumi wengi sasa wanakubali kwamba ujasiriamali ni kiungo muhimu katika kukuza na kuendeleza uchumi wa taifa,ujasiriamali ni njia mbadala ambayo ya kuongeza nafasi za ajira. Katika nchi zinazo endelea biashara ndogo zilizofanikiwa ni msingi ni msingi katika kuongeza ajira,kuongeza kipato na kupunguza umasikini, hivyo basi ni wajibu wa serikiali kusaidia wajasiriamali wakubwa kwa wadogo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa na huduma kwani hatua hiyo itatoa mchango chanya katika mipango ya maendeleo ya nchi au Taifa husika.



MJASIRIAMALI NI NANI? (sifa za mjasiriamali)

  • Ni mtu ambaye anaanzisha na kumiliki kampuni
  • Ni mtu ambaye yupo tayaria kuthubutu
  • Ni mtu ambaye ni mbunifu
  • Ni mtu jasiri asiye ogopa kufeli au kushindwa
  • Ni mtu ambaye kilasiku anatafuta njia mpya za kuzalisha na kuleta upya na mabadiriko
  • Ni mtu mvumilivu
  • Ni kiongozi
  • Ni mshindani asiyekata tamaa
  • Ni mtu ambaye anapenda kuwajibika na kazi kwa bidii
  • Ni mtu anayetazama maisha ya mbele
  • N mtu ambaye anaweza kubadirisha na kutumia nafasi kama fulsa. 
  • Ni mtu ambaye anahitaji na anahamu ya mafanikio
  • Ni mtu ambaye anaweza kujitegemea.

Je wewe unasifa hizo hapo juu? 

Lakini sio lazima uwe nazo zote zilizo orodheshwa hapo juu, hata sifa chache tu zina kufanya uwe mjasiriamali. kitu cha kuzingatia ni kwamba baadhi ya sifa mtu huzaliwa nazo na zingine mtu hujifunza tu, hivyo nawe unaweza jifunza na ukawa mjasiriamali mkubwa na mwenye mafanikio.


JE UPOTAYARI KUWA MJASIRIAMALI?

Kama unata kuwa mjasiriamali basi jibu maswali yafuatayo, kama majibu yako yatakuwa ndio basi wewe ni mjasiriamali lakini kama majibu yako hayatakuwa ndio basi unaweza kujipanga upya na ukatafuta namana nyingine ya kueweza kuwa mjasiriamali labda kwa kujifunza dhana za ujasiriamali.


MASWALI YA KUJIULIZA

1.Je umejiandaa kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo?


2. Je upo tayali kukumbana na kutatua matatizo na changamoto?


3. Je unayafahamu vizuri mazingira unayoishi na je upo tayari kuyatumia na kuanzisha jambo jipya?


4. Je upotayari kusubiri kwa muda mrefu matunda ya juhudi zako?


FAIDA ZA UJASIRIAMALI

  • Kukuza na kuendeleza uchumi katika nchi.
  • Kupunguza umasikini miongoni mwa watu.
  • Ujasiriamali hutusaidia kutumia ipasavyo rasilimali tulizonazo. 
  • Matumizi sahihi ya rasilimali watu.
  • Ujasiamali hutupa mwanga katika kufanya na kuanzisha shughuli mpya ujira binasfsi na nafasi za ajira kwa watu wengi.
  • Hupunguza kiwango cha umasikini miongoni mwa watu. 
  • Hupunguza tofauti katika maendeleo baina ya watu, mikoa, nchi n.k


VITU VINAVYOMJENGA MJASILIAMALI
  1. MTAJI
  2. FURSA
  3. UBUNIFU
  4. MAWASILIANO


MTAJI
Ni kitu chochote ambacho mjasiriamali anawezatumia katika kuzalishia au kufanyia jambo flani kwa lengo la kupata faida. mtaji umegawanyika katika miundo ifuatayo:- mtaji wa fedha,nguvu kazi,mtaji jamii,elimu na utaalamu katika jambo flani.

FURSA
Fursa ni kama uti wa mgongo kwa mjasiriamali. mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kutambua au kugundua fursa, uwezo wa kuchambua na kuchanganua fursa pia kuchukua hatua juu ya fursa husika.

UBUNIFU
Kwa kawaida mjasiriamali anatakiwa kuwa mbunifu, ubunifu ndio unamtofautisha mtu mmoja na mwingine hata kama wote watafanya jambo linalo fanana. kilasiku unatakiwa kufikiri ni jinsi gani utafanya jambo jipya ua jambo lililofanya na wengine lakini wewe ufanye katika njia tofauti.

MAWASILIANO

Mawasiliano huunganisha vitu pamoja ana huweka watu pamoja na husaidia kupata taarifu huhimu katika biashara yako.Mawasiliana huunganisha mtaji, fulsa na ubunifu, mjasiriamali anatakiwa kuboresha mawasiliano ili afanikiwe katika ujasiliamali wake

Chanzo; http://www.morrismshota.com/2014/07/ujasiliamali-ni-nini-chimbulko-lake-na.html

No comments:

Post a Comment